VIJANA WAASWA KUENZI NA KUENDELEZA AMANI NCHINI

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wa kwanza kulia akifungua pazia kushiria kuzindua rasmi Kavazi la Mwalimu la Mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Profesa Issa Shivji.

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wa kushoto akifungua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi chapisho namba 4 la Kavazi la mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam kushoto ni Profesa Issa Shivji

Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghalib Bilal wa pili kushoto akifatilia kwa amakini mdahalo wakati wa  ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam

………………………………………………………………….

Na Ally Daud- MAELEZO -Dar es Salaam.

VIJANA wametakiwa kuienzi na kuendelea kuitunza amani iliyoachwa na  waasisi wa taifa ili kuijenga Tanzania yenye amani na utulivu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na baadaye.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakati wa ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa Mwalimu Nyerere uliojadili maendeleo ya elimu ya juu Afrika ulioambatana na ufunguzi wa hifadhi ya nyaraka ya Mwalimu Nyerere.

Jaji Warioba  alisema kuwa vijana wanatakiwa kuenzi na kuendeleza amani iliyoachwa na waasisi wetu kwa kuwa  imejenga misingi bora katika kwa vizazi vya Watanzania.

“Vijana ni nguvu kazi ya taifa hivyo mnapaswa kuitunza na kuendeleza amani ambayo imeachwa na waasisi wa taifa kwa maendeleo ya nchi yetu” amesema Jaji. Warioba.

Aidha Jaji Warioba alisema kuwa vijana waache kutumia muda wao kuzungumzia na badala yake watumie nguv na akili kufanya maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla ili kuijenga nchi.

Kwa mujibu wa Jaji Warioba alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha umoja na mshikamano ili kuondokana na ubaguzi wa rangi, kabila, vyama vya siasa na dini na kupigana na maadui watatu wa umasikini, ujinga na maradhi.

Mbali na hayo Jaji Warioba aliwataka kuwa wanasiasa nchini kuwa msaada mkubwa wa wananchi badala ya wananchi kugeuka msaada kwa wanasiasa.