UZINDUZI WA KAVAZI LA MWALIMU NYERERE (LAUNCH OF NYERERE RESOURCE CENTRE)-MACHI 18,2015

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa azindua rasmi Kavazi la Mwalimu NYERERE Jijini Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu  nchini Tanzania Mh. BENJAMIN MKAPA amezindua rasmi Kavazi la Mwalimu Nyerere,kituo huru kilichoanzishwa ndani ya Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania chenye majukumu makubwa matatu.
Jukumu la kwanza ni kuhifadhi nyaraka zilizokusanywa na waandishi wa Bayografia ya Mwalimu NYERERE ili zitumiwe na watafiti na pili ni kutoa nafasi ya mijadala ya kizuoni na mikakati juu ya masuala muhimu ya jamii.
Pili kuandaa na kuendesha mafunzo ya nadharia na mbinu za utafiti  wa masuala ya maendeleo.